22 August 2014

Habari njema: SoundCloud yaanza kuwalipa wasanii

Kampuni ya SoundCloud imesema leo kuwa itaanza kuwalipa wasanii na makampuni ya muziki ambayo nyimbo zao zitawekwa kwenye mtandao huo na kusikilizwa au kupakuliwa ikiwa ni hatua ya kutaka kushindana vikali na YouTube na Spotify.

Mtandao huo ambao hupata watu zaidi ya milioni 175 kwa mwezi wanaosikiliza nyimbo za wasanii, umepanga kuweka matangazo ili kupata mapato ambayo yatagawanywa kwa wanamuziki na kampuni hiyo.
Mwanzilishi wa kampuni hiyo, Alexander Ljung, ameiambia Associated Press kuwa wasanii watakuwa na uwezo wa kuchagua aina ya matangazo kati ya audio au display yatakayoambatana na wimbo wao.
Ljung amesema kwa kuanza kampuni hiyo inaanza kuwalipa wasanii ambao nyimbo zao zinasikilizwa Marekani tu na idadi ya watu waliosikiliza itahesabiwa kupata kiwango cha malipo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname