Nyota wa muziki wa kizazi
kipya, Ramadhan Shaban 'Wabibi' akitega 'mingo' kujiopolea machangu
maeneo ya Sinza Africasana jijini Dar.
Wabibi
anayetamba na kibao chake cha Kitenge kwenye vituo mbalimbali vya redio
na runinga nchini, usiku wa saa saba alikuwa akivinjari katika viwanja
hivyo, akichagua kama wafanyavyo wateja wa nguo dukani. Mara baada ya kuonekana kwa msanii huyo katika viwanja hivyo, chanzo chetu ambacho ni kikereketwa cha maadili, kilipiga simu katika ofisi za Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kitengo kilicho chini ya Global Publishers saa saba usiku kikiripoti skendo hiyo ya aibu.
Msanii Ramadhan Shaban 'Wabibi' akipatana bei na mmoja wa machangudoa.
Bila
kuchelewa paparazi wetu alifika eneo la tukio kwa pikipiki na kumkuta
staa huyo akiendelea na chaguachagua yake kwa akinadada waliovalia
kihasara ili kuwavutia wanaume wakware.Mwanga wa kamera zetu hata hivyo haukuonekana kumshtusha sana msanii huyo ambaye alijichekesha na kujifanya kuendelea na shughuli nyingine, kama walivyokuwa wakifanya watu wengine katika eneo hilo linalosifika kwa biashara ya ukahaba jijini Dar.
Ramadhan Shaban 'Wabibi' akiwa na changudoa mwingine.
Baada
ya kujipatia picha za kutosha za tukio hilo na kuondoka eneo hilo,
makamanda wa OFM hawakwenda kulala, bali waliendelea na uchunguzi wao
katika mitaa mbalimbali.Katika hali isiyotarajiwa, saa mbili baadaye,
msanii huyo kwa mara nyingine alikutwa na OFM akiwa anaendelea na biashara yake ya sagulasagula ya machangudoa, lakini hivi sasa akiwa amehamishia kambi katika eneo la Sinza ya Mapambano.Akiwa amevutiwa na mwanadada mmoja na kuanza kufanya naye mapatano ya bei, paparazi wetu alimuwahi kwa kumpiga picha, ambapo safari hii alishtuka zaidi na chapchap, akachukua Bajaj na kutokomea.
'Wabibi' akikurupushwa na kamera zetu za Global katika eneo la tukio.
Wabibi aliwahi kuwa memba wa kundi la muziki la Suba Mkole, akijulikana kama Wambua Classic ambao walitoa albamu iliyotamba kwa jina la Sonde
No comments:
Post a Comment