Wakati kamati zikiendelea kufanya kazi yake kwenye bunge la katiba
Dodoma, bado kumekua na mvutano kuhusu bunge hilo kuendelea au
kutoendelea kutokana na Wajumbe wa UKAWA kukosekana.
Wakati hayo yakiendelea kuna ripoti imetoka kwenye gazeti la Mtanzania, ikisema:
bunge hilo sasa kuburuzwa Mahakamani kesho August 19 2014 na chama cha
Wanasheria Tanganyika kikitaka Mahakama kuzuia vikao vya bunge hili
kuendelea hadi muafaka wa taifa utakapopatikana ili kupata katiba bora
kwa Wananchi.
No comments:
Post a Comment