Star
wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya
Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama
rafiki wa Wema…
Diamond
juzi alisema kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda
kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia
fursa aliyonayo sasa.
Kwa
mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza na Mpekuzi jana
kwa sharti la kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona
alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa
hata kidogo huku akibaki kuumia.
“Aunty
alipoona alichoandika Diamond alichia msonyo huoo! unajua maneno ya
Diamond yamejaa ukweli mtupu, yalikuwa kama mkuki kwa Aunty, Aunty ni
mtu wa starehe sana si umeona hata ndoa yake haina uhai, ukweli unauma,
yeye na Wema wanapaswa kujiangalia upya Diamond amempa Wema ushauri
mzuri sababu anampenda”
Chanzo
hicho kilisema kuwa Aunty anataka kukata ukaribu wake na Wema ili
kuepusha maneno kwasababu ameshazoea kuishi kwa kujirusha.
“Urafiki
wa Wema na Aunty muda si mrefu utakuwa kama ule wa Kajala, Aunty
anataka kumuacha Wema na bwana’ke yeye achukue hamsini zake” kilisenma
chanzo hicho
Hata hivyo Aunty alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi hakupatikana
No comments:
Post a Comment