Wakiwa
wenye Nyuso za Furaha.Watangazaji mahiri wa Radio na
Televisheni,Bi.Regina Mwalekwa aliyekuwa mtangazaji wa Radio One na
baadae akahamia Clouds FM/TV na sasa amejiunga na Shirika la Utangazaji
la BBC akiwa na mtangazaji mwenzake kutoka kituo cha televisheni cha
ITV/Radio One Bi.Fatma Almas Nyangasa,kama
walivyonaswa na Camera ya Globu ya Jamii ndani ya viwanja vya maonyesho
ya Saba saba yanayoendelea hivi sasa jijini Dar.Bi Regina Mwalekwa kwa
sasa sauti yake itakuwa ikisikika rasmi ndani ya BBC.Globu ya Jamiii
inamtakia kila lakheri katika kituo chake kipya cha kazi.
Bi.Regina
Mwalekwa akifanya mahojiano na mmoja wa washiriki wa maonyesho ya
biashara ya Kimataifa ya Saba saba yanayoendelea katika viwanja vya
Mwal.Julius Nyerere,jijini Dar.


No comments:
Post a Comment