28 July 2014

HAWA NDO WATOTO 7 WA MSANII WA BONGOMUVI CHEKI BUDI

 Msanii mahiri wa filamu Bongo,Nasoro Awardhi 'Cheki Budi'.
MIPANGO
Chekibudi wewe ni msanii mahiri wa filamu Bongo, je, una mpango gani wa kujiendeleza kwa sasa na uigizaji? Salim Liundi, Dar, 0659601205


CHEKIBUDI:  Asante, kuhusu kujiendeleza ni kwamba kazi zangu zipo nyingi na nitaendelea kutoa zenye ubora zaidi, pia nina mpango wa kufungua kampuni yangu.

VIPI KUTOKA KIMATAIFA?
Kwanza nakupa hongera kwa kufanya vizuri katika gemu ila napenda kufahamu umejipangaje kujitangaza kimataifa? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
   


CHEKIBUDI: Sina meneja kwa hiyo kujipanga kimataifa lazima uwe na meneja ambaye atafanya mipango hiyo, hivyo kama kuna mtu anaweza kunisimamia nitoke kimataifa naomba ajitokeze.
USHAURI
Kaka Chekibudi hongera sana, kifupi unaweza, kikubwa angalia Mungu anataka nini kutoka kwako, tekeleza ili uweze kufikia malengo yako, uko vizuri. Thabit Kiula, Igunga, 0786947474
CHEKIBUDI: Asante sana nashukuru.
KWA NINI KIMYA?
Chekibudi mbona uko kimya sana katika filamu zetu za Kibongo? Unajishughulisha na kazi gani kwa sasa? Hawa Bushir, Dar, 0713455487
CHEKIBUDI: Siko kimya, mbona kazi zangu nyingi mpya zipo mtaani?
ALIACHANA NA MKEWE?
Chekibudi mimi nataka nijue kwa nini ulimuacha mkeo wa kwanza ukaoa mwingine? Chiku Ashery, Tanga, 0712791665
CHEKIBUDI: Tulishindwana kitabia kwa hiyo tukaachana.
HISTORIA
Mimi napenda kujua historia yako kwa ufupi. Martha, Mwanza, 0757721767
CHEKIBUDI: Nimezaliwa Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam. Nimekulia Ilala, nimesoma Shule ya Msingi Kasulo.
Baada ya hapo nikajiunga na Shule ya Sekondari Malikazi Chang’ombe ndipo nikaenda nchini Kenya kwa masomo zaidi.
Mwaka 1997, niliingia kwenye sanaa rasmi katika Kikundi cha Splended, Ilala.
HUYU ANAMZIMIKIA
Chekibudi mimi nakupenda sana siyo siri, je, naweza kuwa wako? Asia, Mwanza, 0754045569
CHEKIBUDI: Mimi nina ndoa tayari.

ASILI YAKE NI WAPI?
Hivi wewe jamaa ni Mkolombia au Mtanzania na familia yako ina asili ya wapi? Ramsey, 0656805643
CHEKIBUDI: Mimi ni Mtanzania, baba yangu Myemeni na mama ni Mzanzibar.

MAFANIKIO
Ni mafanikio gani umeyapata kwenye gemu la sanaa tangu uanze kujishughulisha nayo? Dastan, Arusha, 0753047073
CHEKIBUDI: Namshukuru Mungu watoto wangu wanasoma kupitia sanaa, kujuana na watu wengi, kuwa na usafiri na kujikimu kimaisha.
VIPI KUHUSU CHIPUKIZI?
Mimi naipenda sana sanaa na tayari ninafanya sanaa, unawasaidia vipi wasanii wachanga ili angalau kuwapa mwanga? Fredrick Erick, Dar, 0752800295
CHEKIBUDI: Muvi zangu nyingi huwa nawashirikisha wasanii chipukizi, ikiwa ni njia mojawapo ya kuwasaidia.
WATOTO SABA?
Kaka Chekibudi wewe ni Muislam, je, unajikingaje na maovu yanayofanyika Bongo Movies? Pia vipi kuhusu ndoa? Una mke na watoto wangapi? Mshamu Tungupu, Morogoro, 0783176411
CHEKIBUDI: Kama wanafanya ni wao, mimi nayaepuka mambo hayo Mungu ananisaidia, nina watoto saba, watano wa kwangu wa kuzaa na wawili ninawalea.
VIPI USUMBUFU WA MABINTI?
Kaka nakupenda kwa jinsi ulivyo mzuri na mafanikio kimaisha huwa huringi, vipi usumbufu wa mabinti maana wewe ni mkali? Msomaji, 0754341237
CHEKIBUDI: Sijakutana na usumbufu sana wengi wananipa salamu tu ila mimi ndiyo nawasumbua na hawanitaki kisa nina ndevu nyingi.
YEYE NA ROSE NDAUKA NI WAPENZI?
Eti kaka ni kweli una uhusiano wa kimapenzi na Rose Ndauka? Olesha, Kibaha, 0657075168
CHEKIBUDI: Duh! Hiyo sijawahi kuisikia, Rose ni msanii mwenzangu na ananiheshimu kama kaka yake.

ANA BIFU NA JB?
Wewe ni mkali Chekibudi lakini nasikia una bifu na JB (Jacob Steven). Mika, Dar, 0719199683
CHEKIBUDI: Huo ni uzushi, mimi sina bifu na msanii yeyote

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname