HAKIKA AUNTY EZEKIEL ANA GUNDU NA VIDUME?!MWENYEWE AFUNGUKA...SOMA ZAIDI HAPA...!
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
GUNDU? Baada ya kudaiwa kuwa na gundu kufuatia kila
mwanaume anayeishi naye kuandamwa na majanga, staa wa Bongo Movies, Aunt
Ezekiel Grayson ameibuka na kukanusha madai hayo akisema hayana ukweli.
Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson.
Baada ya maneno hayo kutua katika dawati la Ijumaa Wikienda,
wanahabari wetu walimsaka Aunt ili kumsikia anazungumziaje taarifa hizo
ambapo alitiririka:
“Sina gundu na wanaume jamani, uzuri ni kwamba
kila niliyeishi naye kulikuwa na sababu za msingi za kuachana. Siyo Jack
Pemba wala Hartmann (Mbilinyi).
“Watu wanazungumza tu bila kujua ukweli, hata kwa Sunday Demonte
(mumewe wa sasa), yupo vizuri na hajafungwa kama wanavyosema,” alisema
Aunt.
Miongoni mwa wanaume walioogelea katika penzi la Aunt kisha
kumwagana kwa sababu tofuati ni pamoja na Mwilu Mwilola ‘Silvanus’,
Hartman na Jack Pemba.
No comments:
Post a Comment