28 July 2014

BODABODA ANUSA KIFO KISA, KUKWAPUA SIMU!

 Dereva wa bodaboda anayetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) mara baada ya kunaswa kwa wizi wa simu.

Ule mchezo wa kukwapua vitu na kukimbia umemtokea puani dereva wa pikipiki almaarufu bodaboda aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) ambaye amenusa kifo baada ya kukwapua simu ya bei mbaya ya mrembo aitwaye Zaituni Hamisi.Tukio hilo la aina yake lilijiri majira ya asubuhi wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo kwa mujibu wa mashuhuda bodaboda huyo alikuwa amempakiza mwenzake kisha kumfuatilia mrembo huyo kwa nyuma wakati akitembea kwa miguu pembezoni mwa Barabara ya Shekilango.

Dereva huyo wa bodaboda akiwa kwenye mtaro na pikipiki yake mara baada ya kipigo kutoka kwa wananchi.

Shuhuda huyo alisema kuwa alishangaa kumuona yule jamaa aliyepakizwa akimkwapua mrembo huyo lakini kwa bahati nzuri mmoja wa madereva wa Bajaj aliyekuwa karibu alimuona na kumbananisha pembezoni mwa barabara na hatimaye kuingia mtaroni.Soma zaidi>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname