14 June 2014

LULU AKERWA NA KITENDO CHA NANDO WA BBA KUHUSU KUJINADI KUWA NI DEMU WAKE.. SOMA HAPA.


MTOTO MZURI BONGO MOVIES, ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ AMEIBUKA NA KUFUNGUKA KUWA AMEKERWA NA KITENDO CHA MSHIRIKI WA SHINDANO LA BIG BROTHER AFRICA (BBA) 2013, AMIR KHAN NANDO KUJINADI KUWA ALIWAHI KUWA ‘MTU’ WAKE KITU AMBACHO SI CHA KWELI.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.Akizungumza na paparazi kwa juzikati, Lulu alikiri kuwa Nando aliwahi kumtokea na alimkubalia awe ‘my baby’ wake lakini baada ya kumshtukia kuwa hana nia nzuri, alimpotezea kabla hawajazama kwenye dimbwi la mahaba.

“Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kunipitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz nilishamgundua nia yake, nimemshangaa kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa mpenzi wake labda alivyonitokea na kumkubalia lakini sikufanya naye chochote kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme hivyo,” alisema Lulu.

Juzikati, Nando alidai ‘kutembea’ na Lulu lakini alipobanwa zaidi aliumauma maneno na kudai anampenda na yuko tayari kumuoa kwa sababu ana sifa za kuwa mke (wife material).


Amir Khan Nando akiwa kwenye pozi

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname