20 May 2014

UCHAWI MCHANA KWEUPE!!..NJIWA MWENYE HIRIZI ATIKISA MUHIMBILI

Njiwa aliyetua kwenye kitanda cha mgonjwa na baada ya muda mgonjwa akafariki.
Hofu kubwa ilitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatatu ya wiki iliyopita, baada ya Njiwa mweusi, mwenye miguu myekundu akiwa na hirizi iliyofungwa katika mojawapo ya mabawa yake, kutua katika miguu ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodi namba tatu, jengo la Mwaisela.Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wauguzi wa wodi hiyo ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema tukio hilo lilitokea saa 3.55 asubuhi ambapo njiwa huyo aliingia kupitia dirishani na kwenda kutua mguuni mwa Mwanahawa Ngunda (61) aliyekuwa amelala kitanda namba 7, ambaye anadaiwa kuwa mkazi wa Kimara.
Njiwa huyo aliingia dirishani muda mfupi baada ya mgonjwa aliyekuwa jirani na Mwanahawa, aitwaye Fatuma Musa (45) kurejea wodini hapo akitokea kupata vipimo ambapo alisaidiwa na ndugu zake kupanda kitandani kutokana na kuishiwa nguvu.
Inadaiwa kuwa baada ya kuingia wodini, njiwa huyo alianza kuzunguka na kuleta taharuki kubwa kwa wagonjwa, wauguzi na ndugu waliokuwemo, kiasi cha baadhi yao kukimbia huku wakipiga mayowe, kabla ndege huyo hajaenda kutua miguuni mwa mgonjwa huyo, huku akiwa ametuna na macho yake mekundu yakiwa yanalenga lenga machozi.
Inasemekena baada ya muda, ndege huyo aliruka na kutua dirisha lililokuwa usawa wa kitanda alicholala Fatuma na kuzidi kuwakoroga watu ambao waliamini kuwa ni mambo ya kishirikina. Ndugu wa mgonjwa aliyetuliwa na njiwa huyo, anayedaiwa kuwa ni mama yake mzazi, alikosa amani akiamini jambo baya lingemtokea.

Lakini katika hali ya kushangaza zaidi, mhudumu mmoja wa wodi hiyo alisema wakati watu wakitaka njiwa huyo aondolewe ili kuondoa usumbufu, dada wa Fatuma, aliyejulikana kwa jina la Mwanaisha Musa alimwambia mhudumu kuwa yeye amempenda ndege huyo na anaomba apewe kwani anahitaji kwenda kumfuga.soma zaidi>>>>>>>>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname