MAMBO yameanza!
Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri
Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na kusema alikuwa
mchumba wa marehemu, Ijumaa linakujuza.
Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu Jumanne
‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa
yake haipo sawasawa.
Alisema walianzisha uhusiano lakini
haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala,
wazazi wake walimtembelea.
“Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana
anapiga hodi, akaingia akiwa na begi la nguo. Niliogopa kwani wazazi
walikuwepo na walikuwa hawamtambui.
“Hata hivyo, walielewa yakapita, tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua,” alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji.
Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.
Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao


kwani huyo dada alikuwa anaulazima gani wa kujieleza kiasi hicho, hawezi kufanya jambo akakaa kimya, wanawake tujifunze kuwa na kaba ya roho au waswahili husema mwanamke unatakiwa kuwa na fivua viwili ,hata sijampenda
ReplyDeletemwanamke unatakiwa uwe na vifua viwili cha mbele na cha nyuma ili uyahifadhi mambo yako sio kila jambo ni lazima useme angekaa kimya asingekuwa mtu, huo ni umaarufu wa kishamba,
ReplyDelete