Juventus wako katika hatua nzuri ya ya kutwaa taji la tatu mfululizo la Serie A baada ya kutoka nyuma na kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Sassuolo.
Simone Zaza alimtungua Gianluigi Buffon na kuipa timu yake bao la kuongoza lakini Carlos Tevez akasawazisha.
Claudio Marchisio akafunga bao la pili kalba ya Fernando Llorente kupachika bao la tatu.
Juventus wako pointi nane kileleni huku wakibakiwa na michezo mitatu.
No comments:
Post a Comment