Heshima
za mwisho: Kutoka kushoto, Victor Valdes, Carles Puyol, Xavi na Andres
Iniesta wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili wa Tito VilanovaSKWADI zima la Barcelona usiku wa jana limeuaga mwili wa aliyekuwa kocha wao, Tito Vilanova kabla ya mazishi yake.
Wachezaji
wa kikosi cha kwanza walihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu
katika kanisa la Cathedral mjini Barcelona na kutoa heshima zao za
mwisho kwa Vilanova, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 45
baada ya kusumbuliwa na maradhi saratani.
Mkewe
na watoto wao wawili wa kike pia walihudhuria pamoja na mtoto wao
kiume, Adria, anayechezea akademi ya Barca, na binti yake Carlota,
alilia sana.
Dani Alves (kushoto) na Neymar kulia
+15
Pumzika kwa amani: Tito Vilanova amefariki akiwa kijana wa miaka 45
"Leo tunamuaga mpendwa wetu,"alisema Bartomeu. "Nakuahidi, daima atadumu katika mioyo yetu na hatutamsahau milele,"aliongeza.
Kwaheri: Gerardo Martino (kushoto) na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu pia walikuwepo
Waombolezaji mbalimbali wakiwa kanisani jana
Kipa wa Barca, Victor Valdes akiwasili na 'magongo' yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia
No comments:
Post a Comment