29 April 2014

MAJANGA:HUSNA IDDI KISOMA, MKAZI WA MKOA WA PWANI ATIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUZINYOFOA SEHEMU ZA SIRI ZA MUMEWE KATIKA UGOMVI WA WIVU WA MAPENZI


Jeshi la polisi mkoa wa Pwani linamshikilia Husna Iddi Kisoma (19) , mkazi wa Kisemvule Mkuranga mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kumuua mumewe Jumane Mwalami (21) baada ya kumvuta sehemu za siri na kuzinyofoa kutokana na ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi. 




 Akizungumza na kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku na kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya wawili hao huku kijana huyo akimtuhumu mwanamke huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.SHUKA NAYO ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname