Binti Fauzia akiwa amepozi nyumbani kwao maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.
Binti mmoja aliyetambulishwa kwa jina la Fauzia (jina la mbele lipo), mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia nafasi ya umalkia katika imani yenye utata duniani ya Freemason, Uwazi linakudondoshea.
Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.
Akizungumza
na gazeti hili siku chache baada ya kuokoka akiwa nyumbani kwa baba
yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake.
Alikuja
Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo safari hii ilikuwa
amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito kwa sasa.
Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.
ALIKOTOKEA
Fauzia
alisema kuwa mara ya kwanza hakujua kama amekuwa mwanachama wa
Freemason bali alichojua yeye alijiunga na uchawi wenye ushirika wa
Kahama na Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija
Dar usiku na kufanya mambo ya kichawi kwa watu mbalimbali.
Alisema
siku moja aliambiwa lazima amtoe uhai mama yake mdogo, naye kwa uwezo
aliokuwa nao alifanya hivyo, mama yake mdogo akafa kwa kuugua ghafla.
Baada
ya kifo cha mama yake mdogo, ndipo usiku mmoja bibi kizee mmoja
(alimtaja jina) alimtokea katika ulimwengu wa kiroho na kumwambia
alitakiwa aende kwenye Jiji la Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya
kutambulishwa rasmi na kupewa umalkia mdogo.
No comments:
Post a Comment