06 March 2014

YANGA WATUA MISRI KWA KISHINDO, WAARABU WAHANGAIKA

YANGA TUAPicha na Saleh Jembe.com, Misri
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara na wawakilishi pekee wa nchi katika michuano ya kimataifa, Dar Young Africans tayari wamewasili jijini Cairo kujiandaa na mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Africa utakaopigwa jumapili machi 9 mwaka huu dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo,  klabu ya National Al Ahly.
Taarifa kutoka Misri zinaeleza kuwa baada ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa klabu ya Yanga SC kufika uwanja wa ndege mjini humo, waandishi wa habari walitaka kuzungumza na wachezaji, lakini hakuna mchezaji yeyote aliyezungumza nao kwa sababu maalumu.
Waandishi hao baada ya kuchuniwa na wanajangwani, waliishia kuwapiga picha wachezaji, viongozi pamoja na basi walilopanda kuelekea Katika Hotel waliyokusudia kuweka kambi.
Waarabu wamekuwa na utamaduni wa kufanya fitina kwa timu za kigeni kila zinapokwenda kucheza kwao, lengo likiwa ni kuwaondoa mchezoni wapinzani ili wawafunge kirahisi.SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname