MWIGIZAJI mwenye sifa za kimataifa Evonne Cherryl ‘Monalisa’
amewashukia wasanii nyota wanaojisahau na kujiona kuwa wao ndio wao, na
wanajitaidi kuwabania wasanii wengine wanaotaka kuingia katika fani
hiyo, Monalisa anawashangaa wasanii hao ambao wanataka kumiliki tasnia
hiyo kwa kibali cha nani?
“Tasnia ya filamu kwa sasa imevamiwa na watu wasio na mbele wa nyuma,
tena wenye roho mbaya ambao wanawabania hata wasanii waliotangulia
kabla yao, hivi sisi kama tungewabania wao wasiingie kuigiza leo
wangekuwa nyota? Kuwa msanii nyota si kuwa na majungu, fitina na roho
mbaya,”analalamika Monalisa.
Monalisa anasema kuwa hivi sasa kuna tabia mbaya ambayo inafanywa na
wasanii ambao hajawataja kwa majina, kuwa mara nyingi inapotakiwa
kampuni mpya na kuitaji kufanya kazi ya filamu, wasanii hao wafikapoa
katika kampuni hiyo uendesha vitendo vya chuki, majungu na kuwaponda
wasanii wanaochaguliwa kwa ajili ya kazi husika huku wakijigamba kuwa
wao ndio kila kitu.
No comments:
Post a Comment