MASIKINI wa Mungu mama huyu wa kijiji cha Buhundwe wilayani Rorya mkoani Mara akitambulika kwa jina la Catherine Benedicto, amepokea kichapo kikali toka kwa mwanamke mwenzie aliyetajwa kwa jina la Bi. Tatu Wambura kwa kosa la eti kupitisha ng'ombe kwenye eneo la shamba linalomilikiwa na Bi. Tatu.
Inatajwa kuwa jumatano katikati ya wiki tunayoimalizia majira ya saa sita mchana, Catherine akiwa anaswaga ng'ombe wake wapatao 30 hivi na ushee kutoka nyumbani kwake kuelekea malishoni alipitisha mifugo hiyo katika shamba la Bi Tatu Wambura, ambalo hata hivyo lilikuwa halijalimwa wala halikuwa na mazao yoyote na ndipo alipoonwa na Bi Tatu alivamiwa na kupewa kipigo kikali kilichoambatana na makofi na mangumi hata kumpelekea mwanamama huyo kupata maumivu makali sambamba na uvimbeckatika baadhi ya sehemu zake za mwili hasa jichoni.

No comments:
Post a Comment