Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka. |
Hata hivyo
haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo
katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa
tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa watatu na mmoja alikuwa na
bunduki aina ya SMG.
Raia wakishangaa mwili wa mfayabiashara huo ukiondolowa na polisi |
Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo
hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara
huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine
ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya
Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki
na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha
kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya
biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.
''Niliona
watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa risasi na
kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi kutokea
upande wa mtaa wa gerezani na kisha mlio wa pili wa risasi ulikika
tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "muhindi" na baada ya hapo
kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile begi na
kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga maduka
yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii"
EFD machine ikiwa katika gari la mfanyabiashara aliyepigwa risasi leo jijini Dar es Salaam |
Sehemu ya fremu inayosemekana kuwa ni Duka la Mfanyabiashara aliyepigwa Risasi Leo majira ya saa 12 jioni |
No comments:
Post a Comment