Saa 11 jioni, January 1, mwaka 2014, pande za Coco Beach pamefurika
wakazi wa Dar es Salaam wa kila rika. Eneo zima limenuka harufu ya upya
wa mwaka, furaha na matumaini mapya. Mawimbi ya bahari ya Hindi
yanasikika kwa sauti inayovutia.
Rangi ya bahari ipendazayo machoni inanivuta nijaribu kuyagusa maji. Bahati mbaya sikuwa nimejiandaa kuogelea kama watu wengi niliowaona wakifurahia maji. Nikiwa na familia yangu, nakaa kwenye eneo ilipo baa ndogo na viti vya kukalia kwenye beach hiyo maarufu Dar. Nafurahia
kuona tu jinsi watu wanavyoyachezea maji huku baadhi ya wasichana warembo wakiwa kwenye mavazi ya kuogelea na kuyafanya maumbo yao yatengeneze sumaku kali iliyoyavuta macho ya wanaume wengi waliokuwa wakishuhudia.
Mara akatokea kijana mwenye gita la kienyeji akija uelekeo wetu. Kwakuwa napenda muziki, niliamua kumuita nione anachokifanya. Akaniambia anaitwa Mos P na kwamba kama anataka atumbuize basi malipo ni buku tu.
Hii ndio burudani aliyotupa na nimeona nikuonesha pia na wewe. Hapa alitumbuiza wimbo wa Diamond, Nataka Kulewa na kuonesha ujuzi wa kupiga muziki kwa gitaa la kienyeji lenye nyuzi 3 tu
No comments:
Post a Comment