Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la
Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati
mgumu baada ya Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi
ya mwendesha pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa
hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13
majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake ambapo
walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.
Taratibu za mazishi zilipokamilika
mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji
akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo walitulia lakini
vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele hali
ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.
 |
Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi. |
 |
Kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole |
 |
Marehemu Gabriel Osward Ngalele. enzi za uhai wake |
 |
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani |
 |
Katikati mke wa Marehemu |
 |
Mwili wa marehemu ukiagwa makaburini hapo |
 |
Katika
mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi
wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye
aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara. |
No comments:
Post a Comment