Mh. Katibu MKuu, Chama Cha Demokrasia Na Mendeleo
UFIPA STREET, KINONDONI
S. L. P 31191
Dar es Salaam – Tanzania.
YAH: MASHATAKA YA UKIUKWAJI WA KATIBA, KANUNI NA MWONGOZO WA CHAMA....
Rejea barua yako ya tarehe 26 Novemba 2013 yenye kumbukumbu no C/HQ/ADM/KK/08/31 Iliyoelezea maamuzi yaliyofikiwa na kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha tarehe 20-22 Novemba 2013, kiliazimia kwamba niachishwe nafasi zote za uongozi ninazoshikilia katika chama na kwamba Kamati Kuu iliazimia kwamba hatua zaidi za kinidhamu za kuachishwa ama kufukuzwa uanachama zichukuliwe dhidi yangu kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji za 6.5.2(d), ningependa kuwasilisha majibu ya mashtaka hayo kama ifuatavyo;
1.0 MAELEZO YA AWALI; Napenda kuwasilisha utetezi wangu huku nikiwa napinga utaratibu uliotumika kuandaa na kunifikishia mashtaka husika (Defence Under Protest) kwa sababu zifuatazo;
1.1. Hatua za kinidhamu ambazo kimsingi ni adhabu zimeshachukuliwa na Kamati Kuu kwa mashtaka haya haya ambayo nimepatiwa. Kama barua yako inavyosema na nanukuu maneno yako “Kamati Kuu kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.2(d) ya Kanuni za Uendeshaji Shughuli za Chama (‘Kanuni za Uendeshaji’), iliazimia kwamba muachishwe nafasi zote za uongozi mnazoshikilia katika Chama…” (msisitizo ni wangu). Mheshimiwa Katibu Mkuu; Ni wazi kabisa kwamba adhabu ya kuachishwa nafasi zote za uongozi imeshatekelezwa. Kamati Kuu imeshanitia hatiani kwa makosa haya haya ambayo sasa hivi natakiwa nijitetee. Binafsi siamini kwamba kwa utaratibu huu haki itatendeka na inaonekana kutendeka. Ni vigumu sana kusema kwamba haki yangu ya msingi ya kusikilizwa na kujitetea imelindwa wakati tayari adhabu imeshatolewa na chombo kile kile ninachotakiwa kujitetea mbele yake.SOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment