MREMBO
aliyetajwa kwa jina moja la Ema aliyedai kuwa ni mchumba wa jamaa
aliyemtaja kwa jina la Amri au Mdudu amefumaniwa laivu akisaliti penzi
na mwanaume mwingine.
Tukio hilo la aina yake lilijiri kwenye Makaburi ya Buguruni, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwekewa mtego.
TAARIFA KWA OFM
Wakati
makachero wa Oparesheni Fichua Maovu wakiwa kwenye ‘patroo’ walipokea
taarifa kutoka kwa chanzo chake ambacho kiliomba wafike katika makaburi
hayo ambapo kulikuwa na fumanizi.
OFM: Fumanizi la aina gani? Isije ikawa ni wanandoa tukaingia chaka.
Chanzo: Hawa
bado ni wachumba tu. Jamaa alikuwa anamfuatilia mchumba’ke amemnasa na
jamaa kwenye gari wakifanya mapenzi sasa kuna timbwili zito.
OFM: Una uhakika na unachokisema?
Chanzo: Kama hamtaki acheni (akakata simu).

OFM KAZINI
Kwa kuwa OFM haipuuzii habari, ilimteua ‘kamanda’ wake mmoja ambaye aliwasha bodaboda na kuwahi eneo la tukio.
Huku
sekeseke likiendelea makaburini hapo, Mdudu ambaye alikuwa na jazba ya
kuibiwa ‘mali’ zake alisema kuwa alitonywa na rafiki zake kwamba
mchumba’ke huyo yupo katika Baa ya Kimboka, Buguruni akijirusha na jamaa
huyo.
Mdudu alisema aliamua kwenda katika baa hiyo na kubana sehemu huku akishuhudia kila kitu.
“Unajua nimekuwa nikiambiwa tu kuwa Ema ananisaliti lakini nilikuwa napuuzia.
“Sasa nimeamini baada ya kumshuhudia mwenyewe akisaliti penzi letu,” alisema Mdudu.

VIKAO VYA HARUSI
Alisema kuwa Ema ni mchumba’ke na anaishi na wazazi wake Buguruni-Malapa, Dar na ameshamtolea mahari.
“Ndiyo tumeanza kupanga vikao vya harusi vifanyike katika Baa ya Wazee iliyopo Ilala-Amana (Dar),” alisema.
Alisema
baada ya kuwasubiri hadi usiku wa manane, aliwaona wakiinuka na kuingia
kwenye teksi ndipo na washikaji zake nao wakachukua bodaboda na kuifuata
ile teksi kwa nyuma bila wahusika kushtuka.
WAKUTWA LAIVU
Alisema
walishangaa kuona gari lile likipaki maeneo ya Makaburi ya Buguruni
kisha dereva akatoka na kwenda kusimama mbali kidogo akivuta sigara.
“Machale yakanicheza nikawatonya wanangu kuwa tusubiri kama dakika kumi halafu tukaivamie teksi.
“Baadaye uzalendo ulinishinda ikabidi nikavamie. Ndipo tukawakuta laivu wanavua nguo wakiwa kimahaba,” alisema Mdudu.
Alisema roho
ilimuuma alipomkuta mchumba’ke huyo ambaye anampenda kwa dhati akiwa
katika hali ile, nusura apoteze fahamu na mara baada ya kuwavamia
waliwatoa nje ndipo sekeseke likaanza.
KUMBE NI MSANII!

Wakati mtiti
ukiendelea, yule mwanaume mwingine aligundulika kuwa kumbe ni msanii wa
Bongo Fleva aliyejitambulisha kwa jina la Spince Seseme.
Akihojiwa
kulikoni kufumaniwa na mke wa mtu, Spince alisema hakufahamu kama Ema ni
mchumba wa mtu kwani kama angefahamu asingetoka naye kimapenzi.

Jamaa huyo
aliyeimba Wimbo wa Ayaya akimshirikisha Ali Kiba alidai alifahamiana na
Ema siku nyingi na hawakuwahi kuvunja amri ya sita.
Kwa mujibu
wa mashuhuda wa tukio hilo wanaomjua jamaa huyo, eti amekuwa akitumia
umaarufu wake kupindua uhusiano wa watu na kuapa kumkomesha.
“Kama polisi wakishindwa tutamwendea kwa babu ili ajue cha mtu mali,” alisikika brazameni mmoja.
Hata hivyo,
tukio hilo lilimalizika kwa kila mmoja kukimbilia Kituo cha Polisi cha
Buguruni akidai kupigwa ambapo hadi OFM inaondoka walikuwa wakichukuliwa
maelezo.
No comments:
Post a Comment