28 November 2013

KWANINI BAADHI YA WATU WANACHUKIA MAFANIKIO YA DIAMOND? ...TATIZO NI ‘BEI YA MKAA’....SOMA ZAIDI HAPA

Watu wengine kamwe hawataweza kukusifu au kukubali kwa unachokifanya mpaka pale usipokuwepo kabisa.. Ni ajabu kuwa watu wengine katu hawawezi kuona kile walichonacho; wakionacho pekee ni kile wasichonacho, ni kile wanachokosa. 

Wakati mwingine inahitaji roho ya paka kuendelea na nguvu kufanya kile unachofanya wakati watu wanaendelea kukudhihaki.

Zaidi ya muziki, kuna kitu gani kizuri kinachoitangaza Tanzania nje ya nchi kwa sasa? Tusaidiane kuuchambua ukweli huu unaomezeka kwa fundo la mate la kulazimisha kinywani.
 
Ni lini mara ya mwisho Tanzania imefanya vizuri kimataifa kwenye soka? Hakuna habari njema zaidi ya kuendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu, iwe kwetu hata nje

Ni lini mara ya mwisho mkimbiaji riadha wa Tanzania ameshinda mbio zozote za kimataifa? Hakuna. 

Kimichezo ni kama bado tumeendelea kuwa wasindikizaji tu. Au umesahau jinsi Selemani Kidunda alivyodundwa mwaka 2012 kwenye mashindano ya Olimpiki? Ukitoa mwaka 2005 pale Nancy Sumari alipokuwa Miss World Afrika, ni lini mrembo yeyote wa Tanzania amewahi kuiletea sifa nchi yetu? 

Ni nini hasa kinachoweza kuifanya Tanzania kuipeperusha bendera yake kwenye jukwaa la kimataifa kwa sifa nzuri? Au labda kipindi hiki tumegeuka kuwa mabingwa wa biashara ya dawa za kulevya na Watanzania ndio wamekuwa vinara wa kukamatwa kila kukicha nchi za nje.

Angekuwepo Kanumba na zile jitihada alizokuwa akizifanya, labda tungesema Bongo Movies ilikuwa inaelekea kuwa njia nzuri ya kutupa heshima pia. Lakini tangu afariki, hakuna mwingine anayeonesha dalili za kufanya kile alichokuwa anakifanya na filamu zetu zimeendelea kuwa za nyumbani pekee.

Hivyo, ukiangalia kwa mifano hiyo, ni muziki pekee wenye matumaini ya kuliongezea ‘kiki’ jina la nchi yetu kwenye ‘google search’. Lakini kama muziki ndio unaonekana kuwa kitu muhimu kinachoitangaza Tanzania, mbona wale wanaofanya vizuri kwa kutuwakilisha nje tunawabeza?

Mpaka muda huu, ukimtoa AY, hakuna msanii mwingine wa Tanzania anayevuma kimataifa kama alivyo Diamond Platnumz. Amefanikiwa kiasi cha hivi karibuni kumshirikisha staa wa Nigeria Davido kwenye remix ya wimbo wake, Number 1 na video iliyogharimu si chini ya dola 25,000 iko mbioni kutoka. Amekuwa ni msanii mwenye kujituma, kutake risk na kutochoka kujaribu kufanya kile wengi wamekuwa wakikiogopa kufanya. Lakini bado kuna watu wengi hawaoni anachokifanya na wameendelea kumkejeli.

Wanasema hakuna binadamu aliye mkamilifu, lakini pamoja na kwamba unaweza kumnyonga mnyonge, ni vyema kukumbuka kumpa haki yake. Ni asili ya mwanadamu kuumizwa na mafanikio ya mtu mwingine, na ndio kinachotokea kwa Diamond. Ameendelea kufanikiwa kiasi mpaka anaanza kuwakera wengine. Si kosa kuchukia maisha na scandal zake, lakini si kosa pia kusifia kile anachoifanyia Tanzania

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname