Kamati
ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku imempiga stop
Ismail Aden Rage kuendelea na ubosi katika klabu ya Simba na
kulibadilisha benchi la ufundi isipokuwa nafasi ya meneja Madaktari wa
timu ambapo pia kwa sasa wanamtarajia ZDRAVOK LOGARUSIC kutoka Croatia.
Akizungumza
kwa niaba ya kamati ya utendaji, mjumbe wa kamati ya utendaji Joseph
Itangare amesema wamemsimamisha mwenyekiti kutokana na kufanya maamuzi
yake binafsi bila kushirikisha kamati ya utendaji ikiwemo kutoitisha
vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (1)ya katiba ya
simba.
Kingine
alichosema Itangare ni ‘vilevile mwenyekiti huyo amesaini mkataba wa
kukiuuza kipindi cha Simba tv bila kushirikisha kamati ya utendaji’
Hii picha hapa juu ni Mzee Kinesi ambae namkariri akisema ‘kwa sasa
lazima twende kikatiba, Mwenyekiti kama hayupo ngazi inayofatia inapanda
juu na tunachagua Mjumbe mwingine ili kukaa kwenye nafasi iliyobakia,
kwa muda huu wa matayarisho ya mkutano mkuu ujao mimi nitakaimu kama
Mwenyekiti wa Simba na Swed atakaimu kama makamu Mwenyekiti’ (picha
kutoka kwa salehjembe.blogspot.com)Kwenye sentensi nyingine, Kinesi amesema ‘Mwenyekiti tumemsimamisha lakini tusubiri maamuzi ya mkutano mkuu ambao utafanyika kwa ajili ya marekebisho ya katiba, kuna mengine yamekiukwa hivyo yatawasilishwa kwenye mkutano mkuu tarehe 1 December’
‘Kutokana na timu yetu kutofanya vizuri, tumeamua kwamba benchi la ufundi tulifumue ili tulijenge upya, sasa litaongozwa na kocha aliekua na Gor Mahia ZDRAVOK LOGARUSIC amekubali kuja na ataanza mazoezi tarehe 2 December na kwa pamoja tumekubaliana ndie atakua kocha mkuu, pia tumekubaliana Matola ndio awe msaidizi wake kwa muda, hatumuondoi Simba B moja kwa moja kuhofia kutetereka
source-millardayo
No comments:
Post a Comment