08 November 2013

BIFU JIPYA LAANZA KATI YA SHILOLE NA WEMA, SHILOLE APANGA KUMPELEKA WEMA POLISI. SOMA CHANZO HAPA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2OtxpKGWw5cQd_oPfY4trmyUAEMUkyzutwnb6omQ7hphiVAgp3Om1oX9rrzPEY7jsmI32IFeZTYcNIRRAFfri5-LB4A8gfK5jsV00TbBucflMczVFCF5c3kcu54CqC_GYSWhJLXs_/s640/shilole.jpg
Zuwena Mohammed 'Shilole' ameonekana kupata uchizi kufuatia matusi mazito aliyoporomoshewa mtandaoni baada ya kuweka picha ya baba wa Wema Sepetu na kuandika R.I.P baada ya kutundika picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram akitarajia kuungwa mkono na wadau, wengi walionekana kukerwa na kitendo hicho huku wakimuita mnafiki mkubwa pamoja na maneno mengine makali.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Shilole alisema amesikitishwa sana na kutukanwa na kuonesha kuwa amepata uchizi na kudai kuwa atamshitaki Wema kwani ndiye anayeweza kuwazuia wapambe wake waache kumshambulia.
Wema akizungumzia ishu hiyo alisema, anamshangaa Shilole kwani wanaomtukana wala hawajui na kama ana mpango wa kumshitaki atapoteza muda wake bure.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname