Ikiwa ni wiki moja imepita
tangu video iliyokuwa ikisubiriwa kwa
hamu ya Hamis Mwinjuma aka Mwana FA na Ambwene Yessaya aka AY ya single
yao ‘Bila kukunja goti’ itoke, FA amezungumzia mambo mbalimbali kuhusu
video hiyo.
Kupitia kipindi cha Showtime cha
Radio Free Africa ya Mwanza, FA amezungumza juu ya matarajio aliyokuwa
nayo katika video hiyo na kile walichokipata baada ya kuiona video kwa
mara ya kwanza.
“Always unakuwa na mawazo mengine
unakuwa unafikiria kitu ambacho ungetarajia kitokee kwenye video yako
kwenye wimbo wako mara nyingi, lakini that is the personal perception tu
aah not necessary kile unachofikiria kitokee kitatokea, mimi binafsi
nilikuwa nafikiria kitu kingine kabisa, lakini jamaa kaja na vitu
vingine kabisa kama zile colors nini ah kanichanganyia habari mi naona
vitu vingine ambavyo sikuvitarajia na vitu ambavyo nilikuwa navitarajia
vingine havikutokea, but am all good”. Alisema FA
Upande wa gharama FA hakuwa tayari
kutaja kiasi kilichotumika lakini amesema wametumia pesa nyingi ikiwa ni
pamoja na kumlipia J. Martins gharama ya kumsafirisha kutoka Nigeria
hadi Afika Kusini na gharama zote za kukaa siku tatu nchini humo.
“hilo ni swala ambalo tumekuwa
tunajaribu kuliruka sababu gharama mara nyingi zimekuwa zinaleta
matatizo lakini jua hela nyingi imetumika, imagine kama kumtoa J.Martins
kutoka Nigeria kumsafirisha business class kumuweka hotel ya
Michelangelo …..kwa siku tatu alizokaa yeye South Afica na vitu kama
hivyo”. Aliongeza FA
FA licha ya kutopata kile
alichokitarajia katika video hiyo lakini ameusifia ubora wake ambao
amesema ndio kati ya sababu zilizochangia video hiyo kupitishwa na vituo
vikubwa vya kimataifa kama Trace, MTV Base, na Channel O.
“moja ya vitu vimeniridhisha sana
kwenye hiyo video ni quality yake achana na kila kitu kingine angalia
quality yake, ndio maana imeweza zile Televisheni kubwa za muziki za
Afrika zote tulizokuwa tunazilenga hiyo video imepita, kwahiyo it is a
hundred percent success”.
Kama umeshaiona video ya ‘Bila
kukunja goti imefanyika mazingira ya ndani (studio) FA amezungumzia
sababu za kuamua kubadilisha wazo lao la mwanzo la kufanyia mtaani.
“walitupa mifano halisi wakatuambia
angalia video za nje kwa mfano ukiangalia video za YMCMB na ukiangalia
video za Jay Z, zote zinafanyika ndani, it’s a trend sasa hivi yani
inabidi watu wafanye hivi, kuna video mbili tatu ambazo zinafanyika nje
lakini trend ni kwamba video zinafanyika ndani za dunia, ndo mkondo
umekuwa hivyo. Kwahiyo jamaa aka-make sense si tulikuwa tunafikiri
kwamba tungeweza kufanya mtaani …..”.
Baada ya audio ya Bila kukunja goti
kutoka, FA na AY walitoa mchongo kwa mashabiki wao kujirekodi style ya
kucheza bila kukunja goti na ku upload clips za video hizo katika
mtandao wa youtube, na kuahidi kwamba washindi wangepata nafasi ya
kushiriki katika video hiyo, FA ameelezea sababu iliyokwamisha zoezi
hilo.
“namna pekee ambayo tunayofikiri
labda ni kuwazawadia wale ambao tunafikiri wamefanya vizuri kwenye hili ,
kwa sababu idea ya kutumia dancers ilishakufa wakati tunaenda South
Africa kwasababu gharama na nini hatuwezi kuwasafirisha wale jamaa
wanaofanya video waje kufanya hapa, that’s one lakini pia lile swala la
kwamba video tunataka kuifanya ndani likawa limeondoa ile idea ya kwamba
sisi tunataka dancers, watu wawe wanacheza mtaani bila kukunja goti na
nini….kwahiyo tunafikiria namna ya kufanya na hizi videos, bado videos
zipo na tunajua zinatudai”.
No comments:
Post a Comment