Kanye West na Kim Kardashian
Rais Obama hajali ushawishi walionao celebrities kwa vijana
wa leo. Katika mahojiano ya hivi karibuni na Amazon.com,Obama alisema ushawishi
mbaya kama vile wa Kim Kardashian na
Kanye West haukuweza kumvuruga kiasi cha kutotekeleza azima yake ya ndoto ya
Marekani aliyokuwa nayo tangu utotoni.
Alaumu ushawishi huo
mbaya walio nao na show
za maisha halisi.
Rais Obama
‘American Dream’ ilihusisha vitu vya msingi ni pamoja na kazi
nzuri ambapo watasikia hali ya usalama. Elimu bora ... Watu walidhani kama wakifanya
kazi kwa bidii watafika huko.... sidhani kama watu huwa wanajiambia, 'Nahitaji
kuwa na nyumba ya miraba 10,000'.... Nadhani, pia kumekuwa na mabadiliko katika
utamaduni. Sisi hatukuwekewa mambo wazi kama watoto wa siku hizi. Hakukuwa na dirisha katika
maisha ya matajiri na maarufu. Watoto walikuwa hawafuatilii kila siku nini Kim
Kardashian alikuwa amevaa au Kanye West anaenda wapi likizo na kufikiri kwamba
kwa namna fulani hiyo ilikuwa ni alama ya mafanikio. ' Alisema rais Obama.
No comments:
Post a Comment