01 August 2013

KESI YA WEMA SEPETU YAAHIRISHWA HADI TAREHE 20

Kesi ya jinai inayomkabili muigizaji Wema Sepetu, ya tuhuma za kumpiga vibao vitano meneja wa hoteli ya Mediterano , pamoja na kuharibu mali za hoteli hiyo, imeahirishwa leo hii pia mpaka tarehe 20 mwezi wa nane.
sakata hilo lilitokea siku ya tarehe 4 mwezi wa 4, kesi yake ya kwanza ilisomwa siku ya tarehe 17, na kuahirishwa mpaka leo hii, na baada ya kufika mahakamani leo hii na Wema kukataa mashtaka hayo, kesi imeahirishwa tena mpaka tarehe 20 mwezi wa 8.
“Siku ya kwanza ya keshi hiyo wanaume walikuwa wengi, lakini leo hii imekuwa tofauti, wasichana walikuwa wengi yaani marafiki zake wakiongozwa na Kajala, walifika majira ya saa mbili na robo na waliitwa sehem maalum (chemba) kwa ajili ya kusikilizwa kesi hiyo, na keshi hiyo ilisomwa ila ilihairishwa mpaka tarehe 20/08/2013″ amesema Mwahija (mwandishi wa habari wa kujitegemea).
SOURCE-tzdailyeye

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname