Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi,
(jina linahifadhiwa) ameingia katika kashfa nzito baada ya kurekodi
mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.
Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu
kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya
kufanya
mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.
Video za mfanyabiashara huyo ambazo
zimekuwa gumzo zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya simu hususan
Whatsapp na nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo Stendi Kuu ya
Mabasi Moshi.
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana
anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo
kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta.
Haijajulikana ni nani aliyeingia katika
kompyuta hiyo na kunakili picha hizo ambazo moja ina sekunde 45 na
nyingine inayomuonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo ikiwa na muda wa
dakika nane.
Habari za uhakika zilizopatikana
zimelidokeza gazeti hili kuwa kwa sasa mfanyabiashara huyo pamoja na
mwanamke huyo wametoroka na hawajulikani walipo baada ya kubaini
wanasakwa na polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro,
Robert Boaz alipoulizwa jana alisema ingawa hajaona video hizo, lakini
kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai hivyo watamtafuta
mfanyabiashara huyo.
Kamanda Boaz alisema polisi wanamsaka
ili ahojiwe kuhusiana na video na vitendo hivyo alivyoiita ni vichafu na
kwamba kimsingi anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili kumaliza mambo.
Alitoa wito kwa jamii kufuata maadili ya dini zote ambapo zinawataka binadamu waishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu.

No comments:
Post a Comment