Dar es Salaam. Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), kimeshika nafasi
ya 11 kwa ubora barani Afrika kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa
Shirika la Utafiti wa Kielimu la Cybermetric Lab lenye makazi yake
nchini Hispania.
Utafiti huo unakiweka chuo hicho katika nafasi
hiyo wakati ile ya kwanza inashikiliwa na Chuo Kikuu Kwazulu Natal cha
Afrika
Kusini na shirika hilo limekuwa likifanya utafiti wa namna hiyo kwa vyuo mbalimbali ulimwenguni kwa miaka kadhaa sasa.
Kusini na shirika hilo limekuwa likifanya utafiti wa namna hiyo kwa vyuo mbalimbali ulimwenguni kwa miaka kadhaa sasa.
Ripoti hiyo inabainisha kuwa utafiti huo ulikuwa
ukiangalia masuala ya ubora wa elimu inayotolewa, muonekano, uwazi
katika utendaji na vigezo vyote vilikuwa na alama 50 na kwa Afrika
Mashariki chuo ambacho kimeshika nafasi za juu ni Makerere cha Uganda
ambacho awamu iliyopita kilishika nafasi ya nne.
“Makerere kinatanguliwa na vyuo vitatu vya Afrika
Kusini na ukiacha Kwazulu kinachoshika nafasi ya pili ni Chuo Kikuu cha
Cape Town ambacho kiliwahi kushika nafasi ya kwanza katika utafiti
uliopita na Stellenbosch” inasema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza
kuwa Chuo Kikuu Nairobi kipo nafasi ya 14.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu (UDSM), Profesa Rwekaza
Mukandala akizungumzia matokeo hayo alisema kuwa yanatia faraja laini
hata hivyo anaamini kuwa chuo chake kilistahili nafasi nzuri zaidi ya
hiyo kutokana na jinsi ambavyo kimejiimarisha hivi sasa.
No comments:
Post a Comment