21 August 2013

CHANZO CHA KIFO CHA BIIIONEA ERASTO MSUYA CHA BAINIKA

  
 Wakati polisi mkoani Kilimanjaro wakitangaza kuwashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya bilionea wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya (43), pia wamesema mauaji hayo ni ya kulipiza kisasi katika biashara ya madini.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua waliyofikia katika kusaka waliohusika na mauaji hayo ambayo yalitetemesha miji ya Arusha na Moshi. 
Kamanda wa polisi mkoa wa kilimanjaro Robert Boaz
Msuya aliuawa saa 6:30 mchana kwa kupigwa risasi kando ya barabara kuu ya Arusha – Moshi eneo la Mijohoroni, wilayani Hai karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Agosti 07, mwaka huu na kufa papo hapo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname