27 July 2013
TAARIFA YA UTATA KUHUSU Ally Kiba kukamatwa na polisi UHOLANZI
Siku hizi Tanzania kumekua na mambo meeeengi yanayozushwa au kuanzia kwenye mitandao ya kijamii sanasana facebook na twitter ambapo miongoni mwa makubwa ya wiki hii ni stori kwamba mwimbaji wa Bongofleva Ally Kiba amekamatwa na polisi wa Amsterdam kwa tuhuma mbalimbali na wengine walidiriki kuripoti kwamba ni dawa za kulevya.
Ally Kiba mwenyewe aliandika kwenye page yake ya twitter kama kukanusha lakini ni tweet ambayo haikuwa rahisi kuielewa au kufahamu alichomaanisha kama unavyoona hapa chini..
Ally Kiba akanusha kukamatwa na polisi Amsterdam July 25 2013 1Baada ya hii tweet ilibidi millardayo.com imuendee inbox au DM kumuuliza kama ni kweli alikamatwa ambapo hili ndio jibu lake….
Ally Kiba akanusha kukamatwa na polisi Amsterdam July 25 2013 2
Ally Kiba
Huenda siku kadhaa zijazo Tanzania ikapata sheria mpya itakayokua inadili na watu wanaoitumia vibaya mitandao kama vile kutukana, kuandika uongo na mengine kama hayo… July 26 2013 Wakili Mwandamizi wa Serikali alisema makosa ya kwenye Internet yameongezeka sana Tanzania na hakuna sheria inayodili nayo moja kwa moja hivyo kuna mpango wa kuipata sheria ya hayo makosa .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment