30 July 2013

HUYU NDO MWANAFUNZI WA KITANZANIA ALIYEUNDA NDEGE YA ABIRIA SHUHUDIA HAPA


Picha ya ndege inayoundwa na kijana, Denis
Kijana wa Kitanzania ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Arusha aitwaye Denis, amefanikiwa kuunda ndege ya abiria. Kijana huyo alianza kuiunda ndege hiyo zaidi ya miezi mitatu iliyo pita na sasa ipo katika hatua za mwisho kabla hajaifanyia majaribio.
Hii ni mara ya pili kwa kijana huyu kuunda ndege baada ya kufanya majaribio mengine huko mkoani Mara ambayo yalikuwa na matunda mazuri. Ndege inayo endelea kutengenezwa na kijana huyu ipo katika eneo la Chuo kikuu cha Arusha kilichopo katika mji mdogo wa Usariver karibu na hifadhi ya wanyama ya Arusha (Arusha National Park).
Endapo majaribio ya Denis yakifanikiwa basi atakuwa ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania na Africa kwa ujumla. Ni wito wangu kwa Serikali na taasisi binafsi kujitokeza na kumuunga mkono kijana huyu katika majaribio haya makubwa na yakimapinduzi.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname