13 May 2013

YALIYO JIRI LEO KATIKA KESI YA LADY JAYDEE MAHAKAMA YA KINONDONI, KESI YATAJWA TENA TAREHE 27 MEI.

 Click image for larger version. 

Name: uploadfromtaptalk1368446913692.jpg 
Views: 0 
Size: 52.0 KB 
ID: 93546


MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa
Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu.

Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname