Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika kwa ujumla.
Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru.
Taarifa
iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua Achebe kuwa
mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika kipindi chake,
ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa
wale wote waliomfahamu.
wale wote waliomfahamu.
Rais
wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima
katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo. Alipata
umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha kwanza cha fasihi
kitwaacho 'Things Fall Apart', ambacho alikitunga mwaka 1958
kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.
Kitabu
hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart
kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake katika
jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za mgaharibi na
kijadi.
Alipata
ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani mwaka
1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi ya
mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa katika ajali ya gari.
Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.
Rais
wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima
katika mioyo na akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment