Jeshi la Polisi mkoani hapa limewakamata watu wawili wanaodaiwa kumteka
mtoto kwa madai ya kupata fidia kutoka kwa wazazi wa mtoto huyo. Taarifa
hizo zinasema kuwa mtoto huyo alitoweka nyumbani kwa bibi yake
Februari
27, majira ya saa 4 asubuhi na kwamba baada ya kufanyika kwa operesheni
maalumu kutoka kwa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi, alikutwa akiwa
mikononi mwa mateka hao.“Baada ya kupata taarifa, tuliunda timu maalumu na kuwapata watekaji wakiwa wilayani Rombo, mtego wetu ulinasa na kumkamata Nicholaus Lyimo akiwa amejificha katika Kijiji cha Mashimba, Useri Rombo akiwa na mtoto machakani, tulivyompekua tulikuta vyeti vyake vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kisu,” alisema Boaz.
---
Habari imeandikwa na Fadhili Athumani, Moshi via gazeti la MTANZANIA