shuhuda asimulia jinsi tukio lilivyo tokea...............Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha
na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua
speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.
Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:
Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa rais so akawasimamisha mungu
saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya
kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road
na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na
speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna
magari yanayo-cross from Shekilango.
Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC
badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala
hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona
sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila
baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona
nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia
sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua
si kitu kizuri kutazama.
Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule
mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.
Mdau aliyeshuhudia
No comments:
Post a Comment