28 February 2013

HUYU ndo MTOTO ALIYE TELEKEZWA STAND YA UBUNGO NA MREMBO ALIYESHIRIKI KWENYE VIDEO YA KIDATO KIMOJA.

Mtoto Junior Justine (3) aliyetelekezwa na mama yake mzazi. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo aliokolewa na msamaria mwema.
INASIKITISHA SANA
Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.
“Maya amezaa na kaka yangu Justine anayeishi Marekani na amekuwa akimjali sana kwa kumtumia fedha za matumizi mara kwa mara. Kisa ni kwamba kaka alimwambia Maya ampeleke mtoto Bukoba (nyumbani kwa baba wa mtoto) akasalimie, Maya akakubali lakini akamwambia atapitia kwanza Arusha (nyumbani kwao) ndipo waende Bukoba.
Mrembo Maya Silemwe aliyetelekeza mtoto.
“Justine akamuelewa lakini kumbe alidanganya, hakwenda Arusha na kuna watu walimuona akiingia kwenye klabu moja hapahapa Dar es Salaam, wakamjulisha kaka. Sasa alipompigia kumuuliza, akawa anajing’atang’ata, siku iliyofuata akadamkia Ubungo ili kumsafirisha mtoto kwenda Bukoba kwa mama yetu (bibi wa mtoto) lakini alitaka kumsafirisha kwa kumtumia kondakta,” alisema Monalisa na kuongeza:
“Alikubaliana na kondakta huyo kisha akamwachia namba ya simu ya mama na yake ili waweze kuwasiliana na kumpokea mtoto huko Bukoba.
Kwa bahati mbaya siku ile yule konda alikuwa hasafiri mpaka siku inayofuatia. Mtoto akaanza kuhangaika stendi siku nzima bila uangalizi mzuri
.
“Bahati nzuri mama mmoja msamaria mwema akafuatilia na kuonana na huyo konda, akamuomba namba za mama wa Bukoba kisha akawasiliana naye, kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda huko siku iliyofuata, akaamua kuchukua jukumu la kusafiri naye.”
Monalisa alikubali kutoa namba za simu za msamaria aliyejitolea kusafiri na mtoto huyo, alipopigiwa alikiri lakini aliomba sana asitajwe .
“Mimi kama mzazi iliniuma sana kumuona mtoto mdogo anahangaika stendi bila uangalizi. Nilishangaa sana kuona mzazi aliyeingia ‘leba’ anawezaje kumwacha mwanaye mdogo namna ile asafiri mwenyewe?” alisema.
MSIKIE BABA WA MTOTO
Tulimvutia waya baba mzazi wa mtoto huyo, Justine aishiye Marekani ambapo alisema: “Jambo hilo limeniumiza sana. Kwa kweli kama ningekuwa huko nyumbani (Bongo) ningehakikisha namfundisha adabu huyo mwanamke kupitia sheria.
“Nashukuru kusikia kwamba mwanangu alifikishwa salama Bukoba.”

MAMA WA MTOTO SASA
Mama wa mtoto huyo alipopigiwa simu alizua kioja baada ya kukataa kwamba hajawahi kumuacha mtoto kwa konda Ubungo na pia akadai eti hana mtoto na wala hajawahi kuzaa katika maisha yake yote.
Wakati tukijiandaa kwenda mitamboni juzi Jumatatu, habari zilizopenyeza katika chumba chetu cha habari zilisema kwamba mrembo huyo alimpigia simu mama mkwe wake na kumchimba mkwara mzito.

Comments system

Disqus Shortname