25 January 2013

TASWIRA KATIKA PICHA.... VURUGU ZA MTWARA LEO .MWANDISHI CHANEL 10 AJERUHIWA

Kwa hali kama hii serikali inabidi ikae na wanamtwara wazungumze juu ya suala la gesi maana itasababisha machafuko  huko Mtwara na Tanzania  kiujumla.
 Askari wa kutuliza ghasia wakijiandaa kuzuia vurugu zilizotokea Mtwara, leo kwa kile kilinachodaiwa ni mwendelezo wa vurugu za madai ya gesi.


Hii ndio Ilikuwa Mahakama ya Mwanzo Mtwara ikimalizika baada ya kuchomwa na Wananchi wa Mtwara waliokuwa wakizunguka kwa madai mbalimbali ikiwemo Imani za Kishirikina za Diwani,Pamoja na sakata la gesi kwa njia ya Mabomba kutoka Mtwara kwenda Kinyerezi..
191 VURUGU MTWARA: NYUMBA ZA GHASIA, SINANI ZAVUNJWA
Maaskari wakitulia ghasia

 

Katika vurugu hizo, mwandishi wa habari wa Chanel Ten, amejeruhiwa kichwani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Inasemekana Nyumba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia imepigwa mawe na kuvunjwa vioo na Mahakama ya Mwanzo kuchomwa moto  Mtwara Mjini hivyo Jeshi la wananchi limelazimika kuingilia kati kutuliza ghasia hizo.
Aidha imeelezwa kwa katika harakati hizo pia Mahakama ya Mwanzo imechomwa moto na kusababisha askari kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao na kulazimika Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, kuingilia kati kutuliza ghasia hizo.

Comments system

Disqus Shortname