17 December 2012

MWENYEKITI CHADEMA UK ATIMULIWA


i) Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii) Aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi
iii) Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv) Awe na msimamo wa kiitikadi
Kwa hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia leotarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya kitanzania, kama vile: -
i) Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii) Kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
Uongozi unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli, tutaliondoa tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.
“We fail in most of our endeavours because we too often underestimate People’s Power” [M4C UK, 2012]
Na christina George

Comments system

Disqus Shortname