Jocelyne
Maro Mii East Africa Tanzania akipunga mkono kwa mashabiki wake mara
baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa
kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa
Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.
Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza
kushinda taji hilo toka lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye
tmamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota
Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima
ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi
wake.
(PICHA NA KAMANDA WA FULLSHANGWEBLOG)
Miss
Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na Miss Uganda Ayisha
Nagudi mshindi wa pili katika shindano hilo kushoto na Miss Burundi
Ariela Kwizera ambaye alipata nafasi ya tatu katika shindano hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na warembo wenzake alioingia nao kwenye tano bora ya shindano hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akiwa amepigwa na butwaa mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo jana usiku.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipongezwa na wenzake mara baada ya kushinda katika shindano hilo.
Warembo hawa ndiyo walioingia katika tano bora ya shindano la Miss East Africa.
Warembo hawa ndiyo walioingia katika kumi bora ya shindano la Miss East Africa.
MC wa shindano la Miss East Afrca Guetano Kagwa akitangaza warembo walioingia katika kumi bora kwenye shindano hilo.

Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Warembo wakipita na vazi la Ubunifu.

Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.

The Voice Wonder nao wakifunika mbaya.
Mzungu Kichaa akaleta kichaa chake jukwaani na kuwaburudisha vya kutosha watu mbalimbali waliohudhuria katika shindano hilo.