Muongozaji wa filamu maarufu ya Zero
Dark Thirty, Kathryn Bigelow anataraia kuonyesha ujuzi wake katika
kutengeneza filamu kupitia kazi yake mpya ambayo inaelezea tukio zima la
mchakato ambao ulifanikisha kukamatwa na kuuawa kwa kiongozi wa al
Qaeda Osama Bin Laden.Filamu hii itakuwa ikionyesha uchunguzi ambao
umekuwa ukifanywa kwa miaka 10 mfululizo ili kujua mienendo ya Bin Laden
na jinsi anavyoishi pamoja na timu ya makomandoo ambao walisimama
mstari wa mbele hadi kumaliza kazi waliyokuwa wametumwa.
Filamu hii itaonyeshwa kwa mara ya kwanza leo katika baadhi ya miji
ambayo imechaguliwa na itaachiwa rasmi duniani Januari 11 mwakani.