Ommy Dimpoz |
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz amesema kuwa licha
ya kutumia kiasi cha shilingi milioni 5 kurudisha gari yake kwenye hali
ya kawaida hawezi kumchukia msanii mwenzake Lord Eyez anayeshikiliwa
korokoroni hivi sasa kwa tuhuma za kuiba vifaa kutoka kwenye gari yake.
“Nafahamu
kuwa kuwa siruhusiwi kuzungumza lolote kwa kuwa suala liko
Polisi,ninachoweza kukwambia ni kuwa binafsi nimemsamehe Lord na
wenzake, sababu huwezi kujua kuhusu kesho, nimepanga kukutana naye na
kumwambia hili jambo, najisikia vibaya lakini nashukuru kuwa gari yangu
nimeshairekebisha na sasa ndiyo ninayoitumia tena licha ya kuwa
nimetumiagharama kubwa” alisema Dimpoz.