14 September 2012

POLE SANA JINI KABULA:!!!!!!.....MIMBA YAKE ALOPEWA NA BUSHOKE HAIPO TENA

SIKU chache baada ya kuahidi kumzalia mtoto mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Bushoke, mwigizaji wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amedaiwa kupata tatizo la mimba yake kuharibika.

Chanzo chetu kimetutonya kuwa, kuharibika kwa mimba hiyo

kulibainika hivi karibuni huku mwenyewe akieleza kutojua sababu.

“Mwenyewe anadai hata hajui imeharibika kwa sababu gani lakini ukweli ndiyo huo.Hata  alipohojiwa  na Clouds  Tv juzi  alishindwa  kunena ukweli.Kwa sasa hana raha kabisa kwani alishaamua kuzaa lakini ndiyo hivyo tena,”
kimedai chanzo hicho.


Katika kupata ukweli wa habari hiyo, mwandishi wetu amemtafuta Jini Kabula na alipoulizwa juu ya mimba yake kuchoropoka amesema kwa masikitiko:


“Naomba unipigie baadaye nitakueleza kila kitu lakini ni ukweli kwamba ‘mwanangu’ ametoka.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname