Wasanii
wa kundi la Pa 1 wamekamatwa na silaha walizokuwa wakizitumia kwenye
shooting ya filamu yao inayohusu maisha tofauti ya
vijana mtaani. Member
wa PA 1 `Ola ' alisema tukio hilo limetokea mida ya jioni walivyokuwa
wakitoka kwenye shooting ya Movie hio walikutana na Askari maeneo ya
Sinza ,wakasachiwa na kukutwa na silaha hizo. Kabla ya kupata nafasi ya
kujieleza na kabla askari kutambua kuwa zilikuwa silaha feki na
zakuigizia tu PA 1 walijikuta chini ya ulinzi kituoni. Baada ya kukaa
kituoni kwa saa chache waliweza kutoa maelezo kamili kuhusu silaha hizo
na kupata uongozi wa PA 1 ndio wakatolewa kwa dhamani .
PA
1 wametaka mashabiki zao waelewe kuwa kilichotokea sio kitendo kibaya
ila nikutoelewana tu na kwa sasa wapo nje kwa dhamana mpaka watakapo
maliza jambo hilo na Polisi .Fahamu kuwa filamu wanayo fanya PA 1
inahusu maisha ya Gangsters mitaani ,Maisha ambayo wa
tu wengi hawajapitia. Demo ya filamu hio itatoka siku yoyote.
Baada ya Inteview kwenda hewani Kupitia Power Jams ,Ola Aliandika Hivi Kwenye FaceBook.
source-missago
No comments:
Post a Comment