09 September 2012

Ingini ya treni ya reli ya kati yawaka moto.

 
Meneja Uhusiano wa TRL, Midladjy Maez
Ingini ya treni ya reli ya kati iliyokuwa ikitoka ikitoka Dar es Salaam kwenda Tabora iliwaka moto jana majira ya saa 1 jioni eneo la mlima Saranda huko Manyoni mkoani Singida. na kusababisha watu 15 kujeruhiwa. Kati ya majeruhi hao, 13 walitibiwa na ku

Kwa kuwa ajali hiyo ilitokea sehemu yenye kona, abiria wa mabehewa nyuma waliweza kushuhudia ingini moja ya treni hiyo ikiwaka moto. Kwa uoga abiria walianza kutokea madirishani ili kunusuru maisha yao na kupelekea 15 kati yao kujeruhiwa. Wafanyakazi wakishirikiana na abiria walifanikiwa kuzima moto huo.
Kwa mujibu wa abiria, treni hiyo ilianza kuonesha dalili za matatizo toka mwanzo wa safari kwani ingini ilikuwa inazima na kuwaka. Hakukuwa na msaada wowote walioupata kwa muda wote waliokuwa katika eneo la ajali ambapo kuna pori kubwa. Waliendelea kusubiri bila kutangaziwa chochote huku wakiomba dua. Baadhi yao walipoteza mali zao.
Meneja Uhusiano wa TRL, Bw. Midlady Maez alisema uchunguzi zaidi utafanywa kujua chanzo cha ingini hiyo kuwaka moto. Maneno ya abiria siyo ya kuamini sana kuwa tatizo lilianza kuonekana toka mwanzo wa safari kwani wao siyo wataalam wa mambo hayo. Aliongeza kuwa ilichukua takribani masaa mawili hadi abiria hao kuondolewa eneo hilo baada ya ingine moja ya treni hiyo kuvuta ingini iliyowaka moto hadi Manyoni. Baada ya hapo ingini nyingine toka Manyoni ilienda eneo la mlima Saranda na kuvuta mabehewa kuelekea Manyoni. Alisema hadi saa 3 usiku abiria wote walikuwa Manyoni.
Majeruhi wawili walilazimika kulazwa hospitali ya Manyoni kwa matibabu zaidi. Mmoja ni mwanamke ambaye ambaye amevunjika miguu na mwanaume mmoja ambaye alivunjika mbavu na mkono. Majeruhi 13 na abiria wengine waliendelea na safari kuelekea Tabora majira ya saa 8 usiku.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname