Njia ya asili ya kuzuia mimba ni mbinu pekee ambayo wanamama wa miaka ile kabla ya madawa ya kisasa(kizungu) kugunduliwa.
Njia hii inauhakika wa asilimia 96-mpaka 98 kama zilivyo njia nyingine za kuzuia mimba kama vile
vidonge, sindano, patch, Coil.
Njia nyingine asilia ni kumwaga nje (withdrawn), lakini hii unahitaji zaidi ushirikaino wa mpenzi wako, mawasiliano wakati wa tendo kwani akijisahau au kuchelewa ujue kitu na box.
Mipira (Condoms) ndio kinga pekee inayozuia mimba na
magonjwa yote ya ngono kwa asilimia 99 na ile moja iliyobaki ni kwa
ajili ya sababu za kisheria kulinda Makampuni incase mtu akatumia
vibaya na kushika mimba au gonjwa la zinaa. Vilevile Kinga hii (Condom)
ndio pekee ambayo ham-badilishi mwanamke kihomono au kimaumbile.
Njia
ya asili ya kuzuia mimba hutumiwa na wanawake ambao kwa namna moja au
nyingine hawataki kutumia madawa ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya
miili yao kama vile kunenepa, kutokwa na majimaji ukeni na pia kuna
tetesi kuwa yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata Saratani ya Kizazi
na Matiti.
Kuzuia mimba kwa kutumia tarehe inauhakika ikiwa mzunguuko wako ni uleule na sio mrefu (siku 32-35) wala mfupi (siku 18-24) bali ni ule wa kawaida ambao ni siku 28.
Ili
kutumia mtindo/mbinu hii ya kuzuia mimba unapaswa kuanza kuhesabu siku
zako sasa na fuatilia kwa karibu mzunguuko wako na kuhakikisha kuwa
una siku 28 sio chini wala juu ya hapo.
Kwa
kawaida unaaza akufuatilia kwa miezi mitatu hadi sita (kama umewahi
kutumia madawa ya kuzuia mimba) kabla hujaanza kuitumia njia hii.
Namna ya kuhesabu
Ili
kuwa na uhakika na urefu au ufupi wa mzunguuko wako unapaswa kuhesabu
siku ya kwanza utakayo ona damu mpaka utakapo ona damu ya mwezi utakao
fuata.
Mfn; leo tarehe 9 mwezi wa nane ndio umeanza hedhi basi hedhi ya mwezi ujao itakuwa tarehe 7 mwezi wa tisa.....hii ni kama mzunguuko wako usiobadilika (sio mrefu au mfupi) ambao ni siku ishirini na nane tu.
Siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya tisa ni salama na huwezi kushika mimba.
Baada ya hapo mpaka siku ya kumi na nne (yai linapevuka) unakuwa hatarini.
Siku ya kumi na saba mpaka siku ya ishirini na mbili unakuwa salama tena mpaka siku ya ishirini na tatu mpaka ishirini na saba (yai pevu linashuka) hatarini
Lakini ile ya ishirini na nane siku ya hedhi nyingine unakuwa salama tena......
Ili kuwa na uhakika kuwa uko kwenye mstari kuliko kuegemea kwenye tarehe tu unatakiwa kujua mabadiliko ya mwili wako.
Unapokuwa
hatarini kushika mimba mara nyingi utahisi nyege zaidi n avilevile
utoko wako utabadilika na kuwa mlaini zaidi (kama lotion) na wakati
mwingine utahisi ute unatoka (ule kama udenda/mlenda)....ukiona hivyo
hakikisha unatumia Condom vinginevyo utashika mimba.
Unapokuwa
salama mara nyingi hamu ya kungonoka inakuwa haipo sana unless
"uchokozwe", vilevile utoko wako unakuwa mzito (kama cream/mafuta
mazito)na mweupe sana yaani hata wakati wa kujiswafi inakuwa taabu na
inaweza kukuchukua muda mrefu zaidi.
Hali ikiwa hivi ujue uko salama kusex bila kinga ya kuzuia mimba.

No comments:
Post a Comment