Stori
kutoka Kinshasa Congo DRC zimetoa uthibitisho kwamba mwanamuziki
maarufu ambae jina lake lina uzito ndani na nje ya Afrika Koffi
Olomide, amehukumiwa kwenda jela kwa miaka
mitatu au kulipa faini.
mitatu au kulipa faini.
Kilichomfanya apigwe hizo nyundo ni fujo alizozifanya akiwa kwenye hoteli moja maarufu Congo DRC pamoja na kumpiga meneja wake.
Nimemsikia
mwandishi wa DW kutoka Congo akisema Koffi alikua akitetewa na zaidi
ya mawakili 15 ambapo mamia ya mashabiki wake walihudhuria Mahakamani
kusikiliza kitatokea nini kwenye kesi yake August 16 2012.
kabla
ya kufikishwa Mahakamani Koffi alikamatwa na polisi August 15 jioni
muda mfupi tu baada ya kufanya fujo hizo na kuwekwa kwenye rumande ya
mahakama ndogo Kinshasa kutokana na makosa aliyofanya hotelini ikiwa ni
pamoja na kumpiga meneja wake ambae amekua akiishi Ulaya.
Mwandishi
wa DW amesema ugomvi huo umetokana na Koffi kumdai meneja huyo euro
elfu sita ambapo mashahidi kwenye eneo la tukio wamekiri kwamba Koffi
alimpiga ngumi meneja wake pamoja na kuvunja mlango wa hoteli.
Hata
hivyo meneja huyo aliwasilisha Mahakamani hoja ya kuondoa mashtaka
yake dhidi ya Koffi na kupendekeza kuwepo kwa maridhiano kati yao
lakini majaji walilipiga chini hilo ombi lake.
Baadhi
ya wananchi waliotoa maoni kuhusu hiyo kesi ya Koffi wameunga mkono
adhabu hiyo na kusema amezidisha, Ulaya ni yeye na kwengine ni yeye,
mwingine amesema ni safi kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa yeye
kutenda kosa.

No comments:
Post a Comment