18 August 2012

Dully sykes: Mimi ni msanii wa kwanza kupanda ndege Tanzania


Dully Sykes hajaacha tabia yake ya kujisifia ndo maana mama yake alimpa jina la Mr. Misifa. Akiongea na Clouds FM msanii huyo mkongwe amesema yeye ni msanii wa kwanza nchini kupanda ndege. Anasema anakumbuka ilikuwa mwaka
2000 alipanda ndege kuelekea Mwanza ambapo alikaa jirani na Joseph Kusaga ambaye alimwambia Dully  asiogope ndege kutokana na kuwa mgeni kwenye chombo hicho.

Dully pia ambaye kwasasa ameongeza aka mbili ‘Superstar na Hunter’ amesema yeye ni superstar wa kwanza Tanzania baada ya Profesa Jay.

Amesema mwaka ambao Profesa aliachia wimbo wa Chemsha Bongo ndio mwaka aliotoa wimbo wake Julietha na kusema yeye ndiye aliyeitambulisha Bongo Flava nchini.

Aliongeza kuwa ameendelea kuwa pale pale na mafanikio yakiongezeka zaidi kutokana na kumheshimu kila mdau wa muziki bila kujali umri wake

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname